Hakika kalimah ya Uislamu ambayo tunaiamini Waislamu, ndio ufunguo wa Pepo. Kalimah ambayo yatakiwa kutamkwa kwa ulimi, kuwekwa ndani ya moyo na kusadikishwa kwa vitendo. Kalimah hiyo ni Laa ilaaha illa Allaah Muhammadun Rasuulu Llaah – Hakuna Mola Apasaye Kuabudiwa ila Allaah na Muhammad ndiye Mjumbe Wake.