Du’aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)
Kuomba Jannah Na Kuepushwa Na Moto Mara Tatu Asubuhi Na Jioni
اللَّهُمَّ إِنِّي أَسْأَلُكَ الْجَنَّةَ وَأَسْتَجِيرُ بِكَ مِنَ النَّارِ (ثلاث مرات)
Allaahumma inniy as-alukal-Jannata wa astajiyru bika minan-naari [mara 3]
Ee Allaah, hakika mimi nakuomba Jannah na najikinga Kwako dhidi ya Moto
Inapaswa kusomwa katika Swalaah baada ya Tashahhud kabla ya kutoa salaam.
[At-Tirmidhiy, An-Nasaaiy, Ibn Maajah – Swahiyh At-Tirmidhiy (2/319) na lafdhi yake ((Atakayemwomba Allaah Jannah mara tatu [asubuhi na jioni], Jannah itasema: Ee Allaah muingize Jannah, na atakayejilinda kwa Allaah na Moto mara tatu, Moto utasema: Ee Allaah mlinde na Moto))